'Wananiambia nimekunywa pombe ndio sababu natetemeka'

Maelezo ya video, 'Wananiambia nimekunywa pombe ndio sababu natetemeka'
'Wananiambia nimekunywa pombe ndio sababu natetemeka'
Iliyochapishwa

Nduta Mbogori, 34, anaishi na ugonjwa wa Parkinson, unaoathiri mfumo wa neva.

Amezungumza na mwandishi wa BBC Asha Juma, na kuelezea safari yake ya maisha.

Nduta Mbogori huanza siku yake na huanza siku yake na kutetemeka na kulazimika kumeza dawa.

Inapoanza kufanyakazi anaanza anaanza kufanya kile alichokusudia kwa siku hiyo.

Ni dhana potofu za aina gani ambazo umekumbana nazo?

Wengine wanasema yeye mlevi, mara ni mraibu wa dawa za kulevya za heroine huku wengine ni uchawi.

Lakini anasema kile ambacho amejuakuna umuhimu wa kuzungumzia anachopitia na ndio ushauri wake kwa wanaopitia changamoto.

"Tafuta mawazo mengine uone kama utapata usaidizi na ukweli ni kwamba, hauko peke yako," anasema Nduta.