Marekani yatumia zaidi ya dola bilioni 37 katika vita dhidi ya Iran

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth amesema vita vinavyoongozwa na Marekani dhidi ya Iran vimeigharimu nchi hiyo takriban dola bilioni 37.5 hadi sasa, ongezeko la karibu dola bilioni 8 ikilinganishwa na makadirio ya awali yaliyotolewa mwezi Mei.

Ruka Video uendelee
  • xx
  • xx
  • xx
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • Dangote
  • xx
  • Lydia Wanjiku

Moja kwa moja

Lizzy Masinga & Mariam Mjahid

  1. Marekani yatangaza kumalizika kwa awamu ya 11 ya mashambulizi yake

    .

    Chanzo cha picha, CENTCOM

    Saa moja baada ya kutangaza kuanza kwa mashambulizi yake dhidi ya Iran, Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM) ilitangaza kukamilika kwa awamu ya kumi na moja ya mashambulizi hayo.

    Siku ya Jumatano asubuhi, wakati mashambulizi hayo yakianza, kulikuwa na ripoti za milipuko kadhaa katika miji kadhaa ya kusini mwa Iran.

    Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha usiku wa kumi na moja , Tehran pia ilishuhudia kuwashwa kwa mifumo ya ulinzi wa anga siku ya Jumatano asubuhi, lakini hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa hadi sasa kuhusu shambulio lolote linaloweza kuwa limeilenga mji mkuu huo wa Iran.

    Miji mingine ambayo iliripotiwa kushambuliwa ni pamoja na Sirik, Chabahar, Bushehr, Mahshahr, Konarak, Tabriz, Behbahan, na Omidieh.

  2. Natumai hujambo na karibu katika taarifa zetu za moja kwa moja